Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa kamanda mwingine wa juu zimetangazwa nchini humo, ambapo majeshi ya Lebanon yamefanikiwa kumwangamiza gaidi huyo wa Daesh “Naifu Al Shaalani” katika mji wa Arsal nchini humo.
Katika mashambulizi hayo majeshi ya Lebanon pia yameangamiza gaidi mwingine ambaye alikuwa pamoja na Amiri huyo na mwingine kati ya aliokuwa nao kutekwa, majeshi ya Lebanon baada ya mashambulizi hayo wameongeza majeshi ya ulinzi katika sehemu hiyo ya Arsal.
Maeneo ya mipaka ya Lebanon na Syria ni katika sehemu ambayo kuna idadi kadhaa ya magaidi wa Daesh, ambapo baadhi ya muda magaidi hao hufanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya Lebanon.
mwisho wa Habari/290